wataalamu kutoka Ten Met wakipokea maandamano mbele ya mgeni rasimi Dkt Nchimbi. |
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoa zawadi ya mipira kwa waalimu wa shule ya Awali ya Nduguti. |
Mkurugenzi wa Bodi ya wanamtandao nchini TEN MET Dr John Karage akitoa taarifa fupi ya wanamtandao na tadhimini. |
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema
Nchimbi amewaomba wanamtandao wa Elimu Ten Met kutoa tathimini ya matokeo ya
kiwanga cha elimu katika maadhimisho ya juma la elimu ya mwakani.
Dr Nchimbi ametoka kauli hiyo wakati akifunga madhimisho hayo
yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida halimashauri ya wilayani Mkalama.
Nchimbi amewaomba TEN MET kutao
tathimini ya elimu katika halmashauri hiyo ya mkalama katika maadhimisho ya
mwaka kesho ilikuonesha hatua ambazo zitakuwa zifikiwa kielimu katika wilaya
hiyo.
Akisoma Risara fupi katika
maadhimisho hayo ya juma laelimu duniani Mkurugenzi wa Bodi ya Wanamtandao wa
Elimu Nchini Dr John karage ameishukuru serikali kwa kuunga mkono maadhimisho
hayo mwakahuu.
Amesema lengo la maadhimisho hayo
nikuweza kufanya tathimini ya hali ya elimu katika maeneo husika na wameamua
kufanya maadhimisho hayo katika wilaya ya mkalama kutokana na matokeo mabaya ya
darasa la saba kwa mwaka jana.
0 Comments