Baada ya mahojiano na Mkurugenzi wa kijiji hicho wanahabari walipata fursa ya kutembelea na kujinea mandhali na maeneo ya kijijihicho cha Nyuki.
Singida
Kampuni
ya Kijiji cha Nyuki iliyopo Kata ya Kisaki mjini Singida inapanga kufungua
ranchi ya uzalishaji wa malkia wa nyuki ili kukabiliana na changamoto ya
upungufu wa makundi ya nyuki inayowakumba wafugaji nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,
Philemon Kiemi, alisema zoezi hilo litaanza mwaka huu kwa lengo la kuongeza
uzalishaji wa asali na bidhaa nyingine za nyuki.
Kiemi
alieleza kuwa wafugaji wa nyuki wamekuwa wakikumbana na changamoto ya
uzalishaji mdogo kutokana na upungufu wa makundi ya nyuki. Ili kukabiliana na
tatizo hilo, kampuni hiyo imejipanga kuwafundisha watu 10,000 mbinu za ufugaji
wa nyuki. Kila mshiriki atapatiwa mzinga mmoja baada ya mafunzo ili kuanzisha
shughuli hiyo.
Aidha,
Kiemi alisema mikakati hii inalenga kuhakikisha rasilimali za misitu na nyuki
zilizopo nchini, hasa katika Mkoa wa Singida ambao umefunikwa kwa kiasi kikubwa
na misitu asilia, zinawanufaisha wananchi kwa kuvuna mazao ya nyuki, yakiwemo
asali.
0 Comments