Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba |
Jeshi la polisi
Mkoani Singida limepanga kufanya doria mara kwa mara na za kushitukiza katika
barabara kuu kwa kutumia vipima mwendo ili kudhibiti madreva wasiotii sheria za
usalaama barabarani.
Akiongea na
waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema hatua hiyo ni
sehemu ya mikakati ya jeshi hilo katika kupunguza ajali za bara barani,
Amesema pamoja na
mambo mengine jeshi hilo litaendelea kufanya ukaguzi kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali na wale wanaokamatwa
kwa kukiuka taratibu wataadhibiwa kwa kufuata taratibu na sheria
zilizoainishwa na serikali.
Sambamba na hilo
amesema wataboresha zoezi la upimaji ulevi kwa madareva hususasani mwanzo wa safari au pale
itakapolazimu kufanya hivyo.
0 Comments