Mbunge wa Singida maghalibi Elibariki Kingu akikabidhi mashuka ya Zahanati kwa diwani mbele ya mkuu wa mkoa wa Singida. |
Mbunge wa jimbo la ikungi magharibi Bw.Elibariki
Kingu amenunua vitanda 34 kwa ajili ya kugawa kwa kila zahanati katika wilaya
ya Ikungi mkoani Singida ikiwa ni moja ya jitihada za kumuunga mkono Rais
Magufuli.
Akizungumza katika mkutano na wananchi Bw.Kingu amesema kuwa vitanda hivyo kwa kila zahanati
itapata vitanda viwili tu ili kupunguza msonagamano wa wagonjwa kulala chini.
Kwa upande mwingine ametoa ahadi kwa mkuu wa mkoa wa
Singida kuwa ndani ya wiki mbili vitanda hivyo vitakuwa vimekabidhiwa kwa kila kata na zahanati.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi |
mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi amemuunga mkono mbunge huyo kwa kuchangia mifuko ya saruji mia moja.
0 Comments