Wakuu wa wilaya na wakurugenzi akipokea vifaa vya kutolea huduma ya Afya baada ya kukabidhiwa na mkuu wa mkoa.
SINGIDA
Mkoa wa Singida
umepokea vifaa maalum vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 178 kwa lengo
la kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa haraka na uhakika. Vifaa hivyo
vinajumuisha pikipiki 11 na gari moja aina ya Centa.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Halima Dendego, alipokea na kukabidhi vifaa hivyo mbele ya Waziri wa
Fedha na Mbunge wa Iramba, Dkt. Mwigulu Nchemba, katika hafla iliyofanyika
kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida. Katika hotuba yake,
Dendego alitoa pongezi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorina
Rudovick, na timu yake kwa juhudi zao katika kuboresha huduma za afya.
Aidha, Mkuu wa
Mkoa alisifu Idara ya Afya ya Mkoa wa Singida kwa kuongoza kitaifa katika
utoaji wa chanjo. Alieleza kuwa vifaa hivyo vitahakikisha huduma za afya
zinafika kwa wananchi katika ngazi ya kata na vijiji kwa ufanisi zaidi.
Baada ya kupokea
vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa aliwakabidhi kwa Wakuu wa Wilaya, Wabunge wa Majimbo
ya Mkoa wa Singida, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wakuu wa Idara ya Afya
walioudhuria hafla hiyo.
"Kwa vifaa hivi, wananchi wa
Singida sasa watapata huduma bora na karibu na makazi yao," alisema RC
Dendego.
0 Comments