Meneja Leseni wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Aridhini (LATRA) Leo Ngowi Makao Makuu akitoa Elimu kwa Mawakala wa Mabasi Mkoa Singida
Singida
Serikali
kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeanza kutoa mafunzo
maalum kwa mawakala wanaotoa huduma ya usafirishaji wa abiria kwa mabasi, kwa
lengo la kuboresha huduma za usafiri nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya mafunzo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa
TANROADS mkoa wa Singida, Meneja Leseni wa LATRA, Bw. Leo Ngowi, amesema
mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha mawakala wa mabasi kuendesha shughuli zao
katika mazingira bora na yenye tija.
"Lengo letu ni kuhakikisha mawakala wanapata uelewa wa kina
kuhusu mfumo wa usimamizi wa usafirishaji wa abiria ili kuboresha huduma kwa
wananchi." – Bw. Leo Ngowi.
Mawakala
wa mabasi kutoka mkoani Singida waliopata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo
wameeleza kuwa elimu hiyo ni muhimu sana, lakini wametoa wito kwa LATRA
kuhakikisha wamiliki wa mabasi nao wanapewa elimu hiyo ili waelewe mfumo mzima
wa usimamizi wa huduma hizo.
"Ingekuwa vyema kama wamiliki wa mabasi nao wangepata mafunzo
haya ili tuwe na ushirikiano mzuri." – Mmoja wa mawakala wa
mabasi.
Semina
hiyo ya siku moja imewakutanisha mawakala wa mabasi kutoka stendi mbalimbali za
abiria na baadhi ya wamiliki wa mabasi kutoka Singida mjini, ikiwa ni hatua ya
kuimarisha huduma za usafiri wa abiria kwa mabasi nchini.
0 Comments