Halmashauri ya wilaya ya Singida imetakiwa
kuharakisha mchakato mapema wa kujenga soko la kimataifa la vitunguu kwa lengo
la kuondoa mkanganyiko ulipo hivisasa baina ya manispaa ya Singida pamoja na
Halmashauri ya wilaya.
Mkuu wa wialaya ya Singida bw, Elias John Tarimo
amesema ilikuweza kudhibiti mkanganyiko uliopo baina ya manispaa ya Singida
na halmashauri ya wilaya ya Singida ni
kujenga soko hilo katika mji mpya wa Meriaya uliopo ndani ya halmashauri.
Amesema lengo la kujega soko hilo hakuleti tafsili ya
kuinyanganya manispaa matao yake.
Katika hatua nyingine bw, Tarimo amewapongeza
wananchi kwa kulima mazao mbalimbali yatakayo saidi halmashauri na mkoa
kujitege kwa chakula pamoja na kupata mapato mbalimbali.
0 Comments