Na:Grace Gwamagobe
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Mkuu wa Mkoa wa Songwe,
Brigedia Jenerali Nicodemas E. Mwangela;
Ninawapongeza kwa kuvuka lengo la makusanyo
na kufikia asilimia 104 hii inaonyesha kuwa katika halmashaurii hii Kuna watu
waaminifu, wanaofanya kazi kwa bidiii na waadilifu.
Licha ya pongezi ninazowapa na katika mambo
mazuri mnayoyafanya bado kuna dosari kadhaa ndio maana kuna hoja 17 za ripoti
ya CAG.
Ofisi yangu iko wazi endapo mtendaji yoyote
akiwa na lolote ambalo anajua natakiwa nilifahamu ofisi yangu iko wazi masaa 24
siku 7.
Ninaomba ushirikiano wenu na mimi ninaamini
katika ushirikiano kwakuwa mtu mmoja hawezi kufanya mambo yote.
Ili tufanye kazi vizuri malengo
tuliyojiwekea tuyatekeleze kwa muda uliopangwa, suala la muda ni muhimu sana,
watendaji tuweke utaratibu wa kujipangia kila siku utafanya nini na upange muda
wa utekelezaji, hii itatusaidia kuenda kwa kasi.
Kuna tatizo kubwa viongozi tunaletewa
taarifa na takwimu za uongo ambapo tukifika maeneo husika kujiridhisha tunakuta
hali ni tofauti, sasa ninataka tukiomba taarifa mtuletee takwimu za uhakika ili
muweze kuepuka baadhi ya hoja.
Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wataalamu
mkisikia kuna ukaguzi wa ofisi ya CAG mnakwepa kwa visingizio vya ugonjwa,
likizo na ruhusa.
Naagiza wakurugenzi msitoe ruhusa kwa
wataalamu kipindi cha ukaguzi wa CAG mpaka kuwe na sababu za msingi ili
wataalamu kutoka ofisi ya CAG wakija wawakute wataalamu husika ambao wanaweza
kujibu hoja vizuri.
Ninaelekeza kuwa hoja iliyojibiwa mwaka jana
wa fedha isionekane tena kwa mwaka huu wa fedha.
Mkaguzi wa Hesabu
kutoka Ofisi ya CAG Joyce Luena;
Halmashauri ya Tunduma ina kesi zenye
thamani ya bilioni 1.38 sawa na asilimia 35 ya bajeti ya mapato ya ndani,
halmashauri izisimamie kesi hizo kwa umakini ili kuokoa fedha za serikali
pamoja na kusimamia mikataba ili kutojiingiza tena katika kesi.
Halmashauri zizingatie maoni ya Mkaguzi wa
ndani kwakuwa ndiye anayewapa picha halisi ya utendaji wa halmashauri unaendaje
na hivyo kuweza kuzuia baadhi ya hoja.
Watendaji wajikite zaidi kwenye kuzuia hoja
na sio kujibu hoja yaani wasiwe mabingwa ya kujibu hoja bali kuzuia hoja.
Halmashauri iendelee kusimamia mipango ya
makusanyo ya mapato waliyojiwekea ili waweze kukusanya Zaidi wasitegee kwakuwa
walivuka lengo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali
Nicodemas E. Mwangela akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma
(hawapo pichani) wakati wa kujadili ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi wa Hesabu za
Serikali.
Watumishi wa
Halmashauri ya Mji wa Tunduma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia
Jenerali Nicodemas E. Mwangela (hayupo pichani) wakati wa kujadili ripoti ya
Mthibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.
0 Comments