Mtoto Antony akisajiliwa shuleni Same- Kilimanjaro baada ya kuwasil |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngara Bw Aidan Bahana akifurahia jambo na mtoto Antony baada ya kufika mkoani Kilimajaro kabla ya kupelekwa shuleni |
Baada ya kuwasili kwanza walifika katiak Ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga Golden Mgonzo na kutia saini. |
Kilimanjaro: Mtoto Anthony Petro (10) wa wilaya ya Ngara mkoani
Kagera aliyezuia baba yake kuuza shamba, amepokelewa kama mfalme katika wilaya
ya Mwanga mkoani Kilimanjaro baada ya kuwasili katika shule ya Amani Vumwe
English Medium Pre-Primary &Secondary School kwa ajili ya kuanza masomo.
Akipokelekwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mwanga hii
leo Golden Ally Mgonzo alimvisha Anthony mataji ya maua kuonesha upendo na
jinsi wananchi wa wilaya hiyo wanavyomtukuza kutokana na ujasiri wake kama
mkombozi wa familia.
Pia aliimbiwa nyimbo za kumkaribisha akiitwa mtoto shujaa
wilayani Ngara wakiwemo wanafunzi wa shule ya Amani Vumwe, viongozi wa
halmashauri ya Mwanga na Ngara pia wananchi waliotamani kumuona mtoto huyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mwanga Golden Mgonzo amemuombea
Anthony amani na upendo pamoja na baraka tele kwa njia ya sala akimuwekea
mikono kwamba Anthony awe kiongozi bora ndani na nje ya Tanzania.
Amesema mtoto huyo amekuwa na ujasiri, utiii, heshima, juhudi na
kazi ukiwemo shirikiano katika kupogania haki za familia bila kutumia ubinafsi
na uchoyo.
Akitumia mfano wa yai lililozama ndani ya maji mkurugenzi huyo
amewaonesha watu kuwa
Anthony alizama katika dimbwi la umaskini ambapo kupitia ujasiri
wake ameibuka na kupata msaada wenye tunu ya familia.
"Tutahakikisha kipaji chake kinalindwa kwa weledi na
kuelekeza kile kitakachokuwa matamanio ya maisha kwake" Amesema Mgonzo
Afisa Elimu idara ya Msingi wilayani Mwanga Allan Saidi amesema
mtoto huyo ameachwa na atakuwamazingira salama na kwamba atakuwa katika
uangalizi wa mara kwa mara aweze kusoma vizuri kutimiza malengo yake
Amesema idara yake itakuwa ikiratibu maendeleo ya taaluma na
mahitaji yake kama yataweza kupungua halmshauri kupitia idara hiyo itawajibika
kusaidia kutatua changamoto kwa masuala ya kiafya kimwili hata kiakili.
Katika hatua nyingine Afisa ustawi wa jamii wa wilaya ya Ngara
Mussa Balagondoza amemkabidhi mtoto Anthony kwa afisa ustawi wa jamii wa wilaya
ya Mwanga Alex Kameo akidai mtoto huyo hana kovu wala jeraha hivyo atunzwe na
kuangaliwa kwa ukaribu.
Amesema kama shule itamtumia katika udadisi alio nao akapata
taaluma ya darasani ataweza kufanya mambo makubwa wasiyotegemea kwani anao upeo
mkubwa ambao wengi wanautegemea kutajwa na kutumiwa na watu wazima.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Aidan
Bahama amewashukuru wakazi wa Mwanga na mmiliki wa shule hiyo kwa mapokezi
ambayo hakutegemea kukuta watu wengi na viongozi mbalimbali
Amesema baada ya kumkabidhi Anthony anakwenda kutafuta wahisani
wa kusomesha dada yake ambapo ameonesha nia mmiliki wa shule ya Rusumo new
Vision English medium kinahosubiriwa ni makibaliano na kutambua masharti
atakayotoa juu yao.
0 Comments