UZINDUZI waCOPA COCA COLA kitaifa yanafanyika mkoani Singida
wakishirikiana na michezo kwa
shule za sekondari Tanzania (UMISSETA )unatarajiwa kufanyika May,05,mwaka
huu katika viwanja vya michezo vya kumbukumbu ya Namfua mjini Singida.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida,Henry Kapera ametoa taarifa
hiyo kwenye ufungaji wa mafunzo ya walimu wa michezo wa shule za msingi na
sekondari yaliyomalizika mjini Singida.
Aidha Kapera amebainisha kwamba Mkoa wa Singida umepewa
kipaumbele kwenye uzinduzi wa michezo hiyo ya COPA COCACOLA kitaifa mwaka huu,na
maandalizi yameanza kufanyika kutokana na Mkoa kupokea wageni wengi na ambao
wataongeza pato la Mkoa wa Singida.
0 Comments