Mkali kutoka pande za Dodoma,Ben Paul amefunguka kuhusiana
na idea ya wimbo wake mpya wa Phone na kusema kwamba ni ngoma ambayo
inazungumzia maisha yake ya kawaida kabisa anayoyaishi katika mahusiano.
Akipiga story na Johflex kupitia kipindi cha Standard Mix
cha Standard Radio Jumanne hii , Ben Paul alisema kwamba yeye mwenyewe huwa na drama za simu katika
mahusiano yake.
“Idea ya phone mimi kwanza kama mimi ninazo drama za phone
kwenye maisha yangu mambo mengi sana tunagombana saa nyingine kwenye mahusiano
kwasababu ya simu kwa hiyo inakuwa hivyo sana’’alisema Ben
Phone ni ngoma ambayo inazungumzia suala la uaminifu katika
mapenzi ambapo Ben Paul amemshirikisha
Mr Eazi kutoka Nigeria.
0 Comments