Mwanamke tajiri zaidi barani Afrika
Isabel dos Santos, bintiye rais wa Angola, amejiongezea utajiri baada ya
kuchukua udhibiti wa benki kubwa zaidi nchini humo.
Bi Santos amechukua udhibiti wa benki hiyo ya BFA baada ya
kampuni yake kununua hisa zaidi katika benki hiyo na kudhibiti zaidi ya
asilimia 50 ya hisa katika benki hiyo.
Hatua hiyo imewaacha waangalizi kutojua ikiwa watamshangilia
mama huyu mjasiria mali au kulalamikia mamlaka na ushawishi wa kiuchumi walio
nao matajiri wachache sana barani afrika.
Isabel dos Santos mwenye umri wa miaka 43, amefanikiwa na angali
na ari ya kufanikiwa zaidi katika kanda ambayo wanaume wanatawala katika ofisi
nyingi za umma na za kibinafsi.
Bi Dos Santos, ni bintiye rais wa angola Jose Eduardo dos
Santos, ambaye ameongoza taifa hilo tangu mwaka wa elfu moja mia kenda na
sabini na tisa.
Ango Katika miaka ya hivi karibuni ilinufaika pakubwa kutokana
na mapato yanayotokana na mauzo ya mafuta na uwekezaji kutoka uchina.
Hata hivyo ufisadi na umaskini vimesalia kuwa changamoto kubwa
zaidi nchini humo.
Bi Dos Santos mara kwa mara amepuuzilia mbali madai kuwa familia
ya rais inapewa nafasi zaidi kuliko raia wengine kuthibiti uchumi na masuala ya
kisiasa ili kuhakikisha kuwa familia hiyo itaendelea kutawala Angola baada ya
rais Dos Santos kustaafu, kama alivyohaidi hivi majuzi.
Kwa sasa Bi Dos Santos anasimamia shirika la mafuta la taifa na
kampuni kubwa zaidi ya kutoa huduma za simu na sasa anadhibiti benki kubwa
zaidi nchini Angola BFA.
Hii ikiashiria kuwa ushawishi wa familia ya rais dos santos
itaendelea kuchukua nafasi kubwa zaidi katika masuala ya kiuchumi na kisiasa
nchini Angola miaka zijazo.la ni moja ya mataifa masikini zaidi duniani.
0 Comments