Bonanza hilo liliambana na michezo mbalimbali ikiwamo Bao,Drafti,soka, mpira wa pete kufukuza kuku,kuvuta kamba,Mashindano ya kula na kunywa pia.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashra Mhe,Exqaud Kigahe akikagua timu ya Mpira wa pete kutoka ofisi ya Ras Mkoa wa Singida.
Mshindano ya kukamata kuu kwa kina mama kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida
Wafanya biashara
na wamiliki wa viwanda wametakiwa kutumia fursa zinazotokana na mashindano ya
kimataifa yanayotarajiwa kufanyika nchini, yakiwemo Mashindano ya CHAN na AFCON
2027.
Akizungumza
kuhusu nafasi za kiuchumi zinazokuja na mashindano haya, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Serera, amesisitiza umuhimu wa
kujipanga mapema ili kunufaika. Aidha, aliwahimiza wafugaji wa kuku wa kienyeji
mkoani Singida kutumia nafasi hii kutangaza ubora wa bidhaa zao, kwani mifugo
hiyo ni maarufu na yenye soko kubwa.
"Mashindano
haya ni fursa muhimu kwa biashara zetu za ndani, na tutumie nafasi hii
kujitangaza kimataifa," alisema Dkt. Serera.
Kwa upande wa
maandalizi, Dkt. Serera alitoa pongezi kwa jitihada za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) katika kuboresha mashindano ya ndani na kuinua vipaji vya
vijana kupitia mashindano mbalimbali.
"Maandalizi
haya yanaenda sambamba na jitihada za kuhakikisha tunakuwa na timu imara
itakayoshiriki Kombe la Dunia 2030. Hii inaanzia katika mashindano ya shule za
msingi, UMITASHUMTA na UMISETA, na ligi za vijana za ngazi ya mikoa na
wilaya,"
aliongeza.
Mashindano haya
yanatarajiwa kuleta mwamko wa kiuchumi mkoani Singida na kote nchini, huku
yakiongeza nafasi ya Tanzania katika ramani ya michezo duniani.
0 Comments