NA JENISTER ZEDEKIA.
Mahakama ya wilaya ya Singida imewasomea mashitaka watuhumiwa 12
wakikabiliwa na kosa la unyanganyi wa kutumia silaha.
Akisoma shitaka hilo shitaka hilo wakili wa serikali Bi.Petrida
Muta amesema kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo mnamo
October,18,2017 majira ya saa nne na nusu usiku katika maeneo ya kititimo
wilaya na mkoa wa Singida.
Bi.Muta amesema washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa
kuliteka gari lenye Namba za usajiri 278 CLY aina ya Scania Bus
kampuni ya Prince Line na kuiba mali mbalimbali za abiria waliokuwemo
katika gari hilo.
Ameyataja majina ya watuhumiwa hao kuwa ni,Rashid
Ramadhani(30),Hassan Musa(33),Benedict Andrea(33),Yohana Issack(24),Yusuph
Adam(45),Musa Said(37),Richard Hassan(30),Hamis Jumanne(33),Mohamed
Siima(46),Mwadi Said(49),Sudi Musa(31) na Michael Andrea(32).
Amesema waliiba vitu mbalimbali ikiwemo fedha,kadi za Bank
na simu ambapo baada ya hapo washitakiwa walifikishwa kituo cha polisi na
kuhojiwa na ndipo walipelekwa mahakamani na kusomewa maelezo ya
onyo ambapo walikana kutenda kosa hilo.
Kunyanganya kwa kutumia silaha ni kosa na kunyume cha sheria
kifungu cha 287A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo
mwaka 2011.
Kwa upande wa wakili katika upande wa mashitaka Tundu Lisu
ameiomba Mahakam iweze kuwaita mashahidi kwa washitakiwa hao wamekaa gerezani
siku 70 na kuomba kesi hiyo iweze kusikilizwa mnamo March,20 mwaka huu.
Hata hivyo hakimu wa mahakama
hiyo Bi.Joyce Minde amehahirisha kesi hiyo hadi March,13 mwaka huu itakapo kuja
kwa ajili ya kusikilizwa kwa upande wa mashahidi na upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika
0 Comments