KANUNI ZA MASHINDANO YA FA ZAWACHANGANYA JKT TZ BAADA YA KICHAPI

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetolea ufafanuzi kuhusiana na kuongezwa kwa dakika thelathini za muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
Hatua hiyo imekuja kutokana na mchezo wa hatua ya nusu fainali uliopigwa katika dimba la Namfua Singida mjini kati ya JKT Tanzania dhidi ya Singida United kuongezewa muda wa dakika 30 badala ya kupigwa matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa mabao 1-1.
TFF imetanabaisha kanuni kuwa zilibadilika ambapo hivi sasa zinaeleza kuwa endapo timu zitatoka sare kwenye raundi ya kwanza mpaka ya sita, mshindi atapatikana kwa kupigiana penati tano kwa tano.
Na endapo zoezi la upigaji wa penati hizo tano halitatoa mshindi, zoezi la upigaji wa matuta litaendelea mpaka pale mshindi akipatikana.
Aidha, kanuni hizo zinaeleza kuwa kuanzia hatua ya robo fainali, timu zikimaliza dakika 90 bila mmoja kupata matokeo, iwe suluhu ama sare ya mabao yoyote ile, dakika 30 za nyongezwa zitatumika kutafuta mshindi wa mchezo huo.
Endapo pia dakika 30 zilizoongezwa hazitapata mshindi, hatua itakayofuata ni ile ya upigaji wa penati tano kwa tano mpaka pale mshindi atakapopatikana pia.
 Uongozi wa Singida United umefurahia kuingia hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga JKT Tanzania kwa jumla ya mabao 2-1 katika Uwanja wa Namfua, mjini Singida, leo lakini ukisema hauhusiki na masuala ya kanuni.
Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, amesema kuwa wao wamefuraha kutinga hatua ya fainali ambapo watakutana na Mtibwa Sugar tarehe pili ya June 2018.
Aidha, Sanga amesema masuala ya kubadilika kwa kanuni wao hawasuki nayo bali wanajali kupata matokeo akieleza hilo linahusika na TFF na si Singida United.
  Sanga ameeleza kuwa hawezi  kuzungumzia hilo na wanachoangalia hivi sasa ni kujipanga dhidi ya Mtibwa kwenye fainali.
"Mimi siwezi kuzungumzia masuala ya kanuni kwasababu hayatuhusu, tnachoangalia kwa sasa ni namna gani tutajipanga kueleka mchezo wa fainali dhidi ya Mtibwa, hayo ya kanuni TFF wanahusika" amesema Sanga.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments