MANISPAA YA SINGIDA IMEJIPANGA KUSAIDIA HUDUMA YA AFYA WATOTO YATIMA SINGIDA

Kulia ni mgeni rasimi Bw Bravo Lyampimbile mkurugenzi wa manispaa ya Singida na kushoto ni Askofu Edward Elias Mapunda wa jimbo katoliki Singida na mlezi wa kituo hicho .ni katika sherehe fupi ya kuukaribisha mwaka mpya 2018 iliyoandaliwa na kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingila hatarishi cha UPENDO HOME kilichopo manispaa ya Singida.
Kulia ni Mratibu wa kituo cha Upendo Home Bw Afesso Wilson Ogenga 


Wageni kutoka Nchini Ujerumani waliyoudhulia katiaka afla hiyo fupi ya kura na kunywa na watoto hao wa Upendo Home.

Bw Bernhard Fries ni mwanzilishi wa kituo hicho (Founder Member of Upendo Home) kituo hicho kimeanzishwa toka mwaka 2008.

Bw Fenny Elisha Mashanjara mlezi na mkurugenzi wa Sumaco Eng.Co LTD akiongea na  wageni waalikwa katika sherehe hiyo.
Meneja wa CRDB tawi la Singida Bw Innocnt Arbogast 








Halmashauri ya manispaa ya singida imeahidi kutatua changamoto zinazokikabili kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo Home kilichoko Manguamitogho.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa manispaa ya Singida Bw Bravo Lyampimbile wakati akijibu Risala iliyosomwa na watoto hao wanaoishi katika kituo hicho.

Miongoni mwa changamoto zitakazotatuliwa ni pamoja na kushugulikiwa upatikanaji wa hati ya kiwanja cha kituo hicho

Bw Bravo amesema kuwa manispaa ya Singida itaendelea kusaidia kutoa huduma kwa watoto wanaishi katika mazingila hatarishi kupitia bajeti ya mwaka huu 2018.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments