Crip fupi ya maneno ya Shekh wa Wilaya ya Singida Shekh Issa Simba.
Taasisi za dini ya Kiislamu mkoani
Singida zimepongeza hali ya amani iliyopo nchini, zikisema kuwa ni matokeo ya
uongozi thabiti wa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake.
Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa
Taasisi za Dini za Kiislamu Mkoa wa Singida, Sheikh Yahaya Hussein, wakati
akitoa salamu katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida,
Godwin Gondwe, katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wake, Sheikh wa Wilaya ya
Singida, Sheikh Issa Simba, amesema kuwa amani iliyopo sasa ni matokeo ya
uongozi bora wa Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Pia ameipongeza
serikali ya mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa Mkoa, Halima Dendego, kwa
kuendelea kuimarisha mshikamano na maendeleo katika mkoa huo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Wilaya ya Singida, Katibu Tawala wa Wilaya, Bi. Naima Chondo, amewataka wazazi
kuwa makini na kuhakikisha watoto wao wanakuwa salama wakati wa sikukuu ya Eid.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Singida iliwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali pamoja na
viongozi wa chama na serikali.
0 Comments