Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo amemteua mbunge wa
upinzani Samy Badibanga kuwa waziri mkuu mpya. Uteuzi huo unakuja kufuatia
makubaliano yenye utata yaliyofikiwa baina ya serikali na makundi ya upinzani.
Taarifa za uteuzi huo zimetangazwa kwa mujibu wa amri ya rais iliyosomwa kupitia
televisheni ya taifa. Badibanga ni kiongozi mkuu wa upinzani katika bunge.
Waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo Augustin Matata Ponyo
alijiuzulu siku ya Jumatatu ili kupisha njia kwa kiongozi wa upinzani kuchukua
wadhifa huo kufuatia makubaliano yaliyopingwa kwa kiasi kikubwa na viongozi
wakuu wa upinzani. Makubaliano hayo yaliyofuatiwa na mjadala wa kitaifa
yalilenga kupunguza mvutano wa kisiasa lakini yatarefusha muda wa rais Joseph
Kabila hadi mwishoni mwa mwaka ujao. Awali, kwa mujibu wa katika alitakiwa
aondoke madarakani mwezi katikati mwa mwezi ujao wa Desemba.
Uteuzi wa Badibanga umekuwa wa mshtuko kwani wengi walimtegema
Vital Kamerhe ambaye aliongoza upande hafifu wa upinzani katika majadiliano ya
kitaifa.
0 Comments