Mbwa wa Polisi akifanya upekuzi katika basi la abiria mjini Singida |
ASKARI wa Kikosi cha Mbwa wa jeshi la polisi Mkoani Singida
akimwongoza mbwa kunusa madawa ya kulevya kwenye moja ya basi (jina
limehifadhiwa) lililokuwa likitoka Mwanza kuelekea Dar-es-Salaam,basi hilo
lililokuwa na madawa hayo ya kulevya lilikamatwa jan.03,mwaka huu 2018,mjini
Singida,.
PICHA Na.06922 Ni Kaimu kamanda jeshi la polisi Mkoa wa
Singida,Mrakibu Mwandamizi,ISAYA MBUGI(wa pili kulia),akifungua kiroba
kilichokuwa na kilo 50 za madawa ya kulevya aina ya bhangi.
Kushoto ni afisa makosa ya jinai Mkoa wa Singida,SSP Stella
Mutahibirwa,akifungua kifurushi kilichokuwa na kilo 50 za bhangi na kwamba
bhangi yenye uzito wa kilo 100,iliyokuwa imekamatwa ilikuwa inasafirishwa
kutoka Mwanza ikipelekwa jijini Dar-es-salaam.
PICHA Na.6935,Ni Kondakta na msaidizi wake wa basi (jina tunalo)
wakiwa wamebeba vifurushi vyenye madawa ya kulevya aina ya
bhangi,wakisindikizwa na askari polisi kitengo cha mbwa,kupeleka kituo cha polisi
cha mjini kati Singida .
0 Comments