UTORO MASHULENI WILAYA YA SINGIDA WAPUNGUA KWA %0.05

Bw Jacob Kateri mtafiti kutoka shirika la ACTIONAID akitoa taarifa ya utafi wa utoro katika shule za msingi wilaya ya Singida



Bi Aggines Aqwilin mratibu wa Shirika la MEDO akifafanua jambo  katika mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa RC MISSIO Singida mjini.

Utafiti uliofanywa na shirika la ACTIONAID kwa kushirikiana na MEDO umeonesha kuwa tatizo la watoto kuacha shule limepungua kwa asilimia kubwa kutoa asilimia 3.9 kwa mwaka 2015 hadi asilimia 0.05 kwa mwaka huu 2017

Hayo yameelezwa na mtafiti kutoka shirika la ActionAID Bw. Jacob Kateri katika utekelezaji wa mradi wa uhamasishaji wa elimu kupitia rasilimali za ndani kwa maana ya kodi katika halmashauri ya wilaya ya Singida.

Akizungumza katika semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wenyeviti wa kamati za shule na vijiji, madiwani na walimu wakuu Bw. Kateri amesema kwasasa tatizo la watoto kuacha shule limepungua kutokana na ushirikishwaji mkubwa kwa wadau wa elimu

Aidha Bw. Steven Mangu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya kijiji cha Kinyamwambo amesema pindi walipopata elimu walikubaliana kuwatoza faini wanafunzi watoro jambo ambalo lilipunguza utoro shuleni hapo

Naye mwenyekiti wa kamati ya shule kijiji cha Mpambaa Bw. Fadhili Mumbee amesema kupitia sheria ndogo ya kijiji ya kupiga faini kwa watoro na wazazi kupeleka taarifa shuleni ya mtoto kutofika shule limewafanya wanafunzi wengi kuhudhuria masomo.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments