JUKWAA LA WADAU WA KILIMO CHA ALIZETI WILAYA YA SINGIDA LAZINDULIWA RASIMI

 Bw. Nasajile Mwambambale kutoka shirika la MIVARF akimaribisha mgeni rasimi katibu tawala wa wilaya ya Singida Bw Wilson Shimo kuongea na wadau hao wa Alizeti kutoka wilaya ya Singida

Katibu tawala  wilaya ya Singida Bw Wilson Shimo akiongea wakati wa uzinduzi wa jukwaa la wadau wa Alizeti. 



wadau wa Alizeti wakichangia wakati wa kuuliza maswali ili kupata ufafanuzi juu ya kilimo cha Alizeti.

Wadau wa alizeti katiika halmashauri ya Singida wametakiwa kujiunga na

jukwaa la alizeti ili kuweza kutimiza malengo yao kimaendeleo hasa kwa
kipindi hiki ambapo Tanzania inatarajiwa kuwa nchi ya viwanda

Hayo yamesemwa na mtoa huduma wa shirika la MIVARF Bw. Nasajile
Mwambambale ambaye alikutana na wadau mbalimbali wa alizeti wakati
wanaunda jukwaa hilo

Bw. Mwambambile amesema jukwaa hili litampa fursa kila mdau wa alizeti
kuweza kufahamiana na wadau wengine ili kurahisisha uzalishaji,
uuzwaji na hata usindikaji wa zao hilo.

Aidha Bw. Mwambambile amesema katika jukwaa hilo zimealikwa taasisi
mbalimbali iliwemo mamlaka za uhakiki wa viwango vya ubora TBS na TFDA
kwa lengo la kuboresha bidhaa zote zinazozalishwa kutokana na zao la
alizeti ili kufikia viwango vya kimataifa.

Naye katibu tawala wa wilaya ya Singida Bw. Wilson Shimo ambaye alikua
mgeni rasmi katika jukwaa hilo amewaomba wazalishaji wa zao la alizeti
kuzalisha zao hilo kwa wingi kutokana na uhitaji mkubwa uliopo katika
viwanda vya usindikaji wa zao hilo

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments