Mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ulinzi shirikishi na wananchi wa Misigiri juu ya ulinzi wa miundombinu ya umeme iliyopita wilayani humo |
Mkazi wa Misigiri akiuliza swali katika mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya kijiji hicho. |
Eng Amos Kaihula mkuu wa njia kuu ya umeme taifa akifafanua jambo. |
Wananchi wa kijiji cha Misigiri wilaya ya Iramba mkoani Singida na vijiji vingine ambapo inapita njia kuu ya msongo wa umeme wametakiwa kuilinda na kuitunza miundo mbinu hiyo ili kuepuka madhara makubwa yatakayotokea ikiwa ni pamoja na vifo pindi utakapo tokea uharibifu wowote
Hayo yameelezwa na Eng. Amosi Kaihula ambaye ni meneja wa njia kuu ya umeme Tanesco Taifa wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Misigiri na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kutunza na kuilinda miundombinu hiyo ya umeme
Eng. Kaihula amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kufungua nati zilizopo kwenye nguzo kubwa zinazopitisha umeme mkubwa jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama pindi ikitokea nguzo imeanguka
Aidha mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Iramba na mkuu wa wilaya hiyo Emanuel Luhahula mapema wakati akiongea na waandishi wa habari amesema serikali haitamfumbia macho mtu yeyote atakaebainika anaharibu miundombinu hiyo ya umeme au kufanya kazi zozote jirani na nguzo hizo
Naye mwananchi mmoja Janeth Lameck ameiomba serikali na viongozi wa kijiji kuweka utaratibu mzuri wa faini atakayotozwa mtu yeyote akibainika kufanya uharibifu na pia kuweka utaratibu wa kumlinda mtu atakayetoa taarifa ya kumfichua muhalifu
0 Comments