mkuu wa wilaya ya Ikungi na kaimu mkuu wa wilaya ya Singida Miraji Mtaturu |
Vitambulisho vya taifa vimetajwa kuwa miongoni mwa haki za
rai na uthibitisho unaonesha kuwa
mhusika anahaki zote katika nchi husika.
Akiongea katika kikao cha wakazi kuhusu zoezi la usajili na
utambuzi kwa wananchi wa manispaa ya Singida Kaimu mkuu wa wilaya ya Simgida
Bw, Miraji Mtaturu amesema vitambulisho hivyo nimuhimu kwa kila mwananchi.
Bw, Mtaturu amesema vitambulisho vya taifa ni alama mojawapo
inayoonesha kuwa na haki katika nchi.
Amesema sasa wakati umefika kwa wananchi kujiandikisha ili
kupata vitambulisho vya taifa ambalo ni zoezi linalotekelezwa na wakala wa
Serikali kupitia vitambulisho vya taifa NDA
Aidha bw, Miraji amewaomba wananchi kutanguliza uzalendo
katika zoezi hilo ili kufanikisha kwa ufanisi uliokusudiwa.
0 Comments