Matokeo ya kushangaza kuwahi kupatikana
katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya yameletwa na Barcelona katika
mechi yao ya marudiano ya ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya
mabingwa wa Ufaransa PSG.
Pengine itachukua miaka kadhaa kuja
kushuhudia hiki walichokifanya Barcelona au ndiyo mwanzo mpya wa timu kuweza
kuiga mfano wao.
Kabla ya mchezo huu Barcelona walihitaji
kupata ushindi wa si chini ya bao 5-0 na kutoruhusu kufungwa goli lolote lakini
hadi mpira unamalizika Barcelona waliibuka na ushindi wa bao 6-1
Magoli matatu ndani ya dakika 7 za mwisho
ndiyo hasa yaliyopeleka kilio kwa PSG Neymar akifunga mawili na Sergi Roberto
ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic akifunga bao la 6 na la ushindi
kwa Barcelona.
Iliwachukua dakika 4 tu Barcelona kupata bao
la kwanza kupitia kwa Luis Suarez kabla ya beki wa PSG Kurzawa hajajifunga na
badae Messi kufunga bao la tatu kwa njia ya penati lakini bao lililofungwa na
Edison Cavani liliwapa nguvu PSG kabla ya kujisahau na kuruhusu kufungwa bao 3
ndani ya dakika 7 za mwisho.
Kwa matokeo hayo Barcelona inaweka rekodi ya
kuwa timu ya kwanza kuvuka hatua hii baada ya kufungwa mechi ya awali zaidi ya
bao 4 na inafanikiwa kupita kwa jumla ya bao 6-5.
0 Comments