Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon
anayeichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani Pierre-Emerik Aubameyang ameibuka
shujaa kwa klabu yake akifunga bao 3 katika ushindi wa bao 4-0 walioupata
Dortmund dhidi ya Benfica.
Dortmund iliyoingia katika mechi hiyo ikiwa
na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 kwenye mechi ya awali ilikua ikihitaji
ushindi tu kuweza kuvuka.
Aubameyang alifanikiwa kufunga mabao yake
dakika ya 4,61 na 85 huku Christian Pulisic akifunga bao moja katika mchezo
uliopigwa kwenye dimba la Signal Iduna Park jijini Dortmund.
0 Comments