Mama Janeth Magufuli akiwasili Manyoni Mkoani Singida |
MKE
wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Pombe Magufuli,Mama
Janaeth Magufuli amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuwatembelea pamoja
na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wanaoishi kwenye vituo vilivyotengwa
kwa ajili ya kuwahifadhi ili wazee hao nao waweze kuishi kama watu wengine.
Mama
Magufuli ambaye amefuatana na Mke wa Waziri Mkuu,Bwana Majaliwa Kassimu
Majaliwa,Bi Mary Majliwa ametoa wito huo alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula
mbali mbali kwenye kituo cha Makazi ya wazee wasiojiweza cha
Sukamahela,wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Amesema
ili wazee hao wanaoishi kwenye makambi maalumu waweze kufarijika na kujiona
wapo sawa na watanzania wengine ni vyema kukawa na mazoea ya kuwatembelea mara
kwa mara pamoja na kuwasaidia na kwamba watakapojenga utamaduni wa kuwasaidia
mungu naye hataweza kuwaacha,ambapo hata hivyo amewatahadharisha kwamba wasije
wakaishia kutoa misaada wakati wa ziara yake hiyo na badala yake misaada hiyo
iwe endelevu.
Awali
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mlata
akiwasilisha salamu za chama amewataja wadau mbali mbali walioungana naye kwa
kuwasaidia wazee hao wakati Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki,Bwana Danieli
Mtuka akiwatahadharisha watu watakaojaribu kubadili matumizi ya msaada huo
uliokabidhiwa kwa wazee hao wasiojiweza.
Mke
wa Rais Dk.John Pombe Magufuli yupo mkoani Singida kwa ziara ya siku moja
ambapo amekabidhi zaidi ya tani saba za vyakula mbali mbali kwenye kituo cha
wazee wasiojiweza cha Sukamahela.
0 Comments