MICHE YA MITI 200 YAPANDWA MANISPAA YA SINGID



Kaimu meya manispaa Singida Yaggi Kiaratu akipanda miti 
Jumla ya miche ya miti ya kivuli 200 imepandwa katika eneo la makaburi ya mwenge yaliyopo katika manispaa ya Singida wakati wa zoezi la usafi mapema leo ili kuhakikisha mazingira yanakuwa katika hali nzuri na salama
Akizungumza katika zoezi hilo diwani wa kata ya Ukombozi .

Bi Yagi Kiaratu amesema pamoja na wananchi wa kata yake kuwa na mazoea ya kupanda pindi katika sehemu mbalimbali wameamua pia kupanda miti eneo hilo la makaburi ili kuweka uzio katika eneo hilo
Amesema jambo hilo lina thawabu kubwa kwani wapo ndugu na jamaa waliopumzishwa na kwamba miti hiyo italeta hewa nzuri na kufyonza hewa chafu ambayo ni hatari kwa afya huku pia akiongeza kuwa miti hiyo itawawezesha wakazi hao nishati ya kuni na kupunguza gharama za maisha

Naye mtendaji wa kata ya ukombozi Edward Salumu amewapongeza viongozi wote wa mtaa wa Mwenge kwa zoezi hilo na kuwaomba waitunze miti hiyo kwani kwa jitihada hizi kutarudisha hali nzuri ya kupata mvua kwa wakati kama ilivyokuwa mwanzo

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments