MABINGWA wa Tanzania
Bara, Yanga, Leo huko Stade De Moroni Mjini Moroni Visiwani Comoro, wamewafumua
Mabingwa wa huko 5-1 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya TOTAL CAF
CHAMPIONZ LIGI ambayo ndiyo Mashindano makubwa kabisa kwa Klabu Barani Afrika.
Hadi Mapumziko Yanga
walikuwa mbele kwa Bao 2-0.
Bao za Yanga hii Leo
zilipigwa na Justin Zullu, 43', Saimon Msuva, 45', Obrey Chirwa, 59', Tambwe,
65', na Kamusoko, 73'
Safari hii Makundi ya
CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF
CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo
yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.
Haya ni Mashindano ya 53
ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI
uanze.
Mshindi wa Mashindano
haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa
Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya
Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.
Bingwa Mtetezi wa CAF
CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Timu hizi zitarudiana
Jijini Dar es Salaam Wikiendi ijayo na Mshindi kutinga Raundi ya Kwanza na
kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda ambazo Jana
zilitoka 0-0 huko Zambia.
Mshindi wa Hatua hiyo
ataenda Makundi.
KIKOSI CHA YANGA: Deogratius Munishi,
Juma Abdul, Mwinyi Haji, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Justin Zullu, Saimoni
Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima
Akiba: Ali Mustafa,
Hassani Kessy, Oscar Joshua, Emanuel Martin, Juma Mahadhi, Juma Saidi, Deusi
Kaseke
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Awali
Ratiba na Matokeo:
Ijumaa Februari 10
KCC – Uganda 1 Primeiro
0
JS Saoura 1 Enugu
Rangers – Nigeria 1
JumamosiFebruaria 11
Zanaco – Zambia 0 APR -
Rwanda 0
Royal Leopards –
Swaziland 0 AS Vita – Congo DR 1
Cnaps Sports –
Madagascar 2 Township Rollers – Botswana 1
Zimamoto – Zanzibar 2
Ferroviario Beira – Mozambique 1
Tusker – Kenya 1 AS Port
Louis -Mauritius 1
Royal Club du Kadiogo –
Burkina Faso 3 Diables Noirs - Congo 0
AS Real de Bamako – Mali
0 Rivers United – Nigeria 0
SS Saint-Louisienne –
Reunion 2 Bidvest Wits - South Africa 1
FC Johansens - Sierra
Leone 1 Fath Union Sport de Rabat - Morocco 1
Côte d'Or – Seychelles 0
Kedus Giorgis - Ethiopia 2
Lioli Football Club –
Lesotho 0 CAPS United FC - Zimbabwe 0
AS Tanda - Ivory Coast 3
AS-FAN - Niger 0
CF Mounana – Gabon 2
Vitalo FC - Burundi 0
US Gorée – Senegal 0
Horoya Athlétique Club - Guinea 0
Jumapili Februari 12
Ngaya Club – Comoros 1
Young Africans – Tanzania 5
17:00 Coton Sport FC –
Cameroon v Atlabara FC - South Sudan
17:00 Gambia Ports
Authority – Gambia v Sewe Sport - Ivory Coast
17:00 All Stars FC –
Ghana v Al-Ahli Tripoli - Libya
17:30 AC Leopards de
Dolisie – Congo v UMS de Loum - Cameroon
19:00 Barrack Young Controllers
FC – Liberia v Stade Malien de Bamako - Mali
19:30 Sony de Ela Nguema
- Equatorial Guinea v El Merreikh - Sudan
0 Comments