Halmashauri ya wilaya ya Singida
imetekeleza Agizo la mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi juu ya
kuhakikisha kila wakuu wa idara za halmashauri kuwa na shamba la Muhogo kuanzia
nusu hekari.
Akizungumza wakati wa kupokea
mbengu za Mhogo kutoka katika chama cha wajasiliamali, wazalishaji wa mbegu
bora za muhogo afisa kilimo umwagiliaji na ushirika halmashauri ya wilaya ya
Singida Bw.Abel Mungale amesema mkuu wa mkoa amepokea mbegu hizo kama ishara ya
shukrani.
Bw.Mungale amesema mizigo hiyo ya
mbegu za muhogo imetolewa kwa baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa
mkoa na mkuu wa wilaya ya Singida.
Kwa upande wake mtendaji wa chama
cha wajasiliamali wazalishaji wa mbegu bora za muhogo kanda ya kati Dodoma na
Singida Bw.Idd Senge amesema wamelima heka 27 za mbegu na zinaendelea kupandwa.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa
Singida Dk.Rehema Nchimbi amemalizia kwa kusema kuwa suala la usalama wa
chakula sio la serikali ni la wananchi wote ikiwemo viongozi kuwa mfano bora.
0 Comments