Nedy Music |
Msanii Nedy Music kutoka katika lebo ya PKP inayomilikiwa na
Mkali wa Kajiandae,Ommy Dimpoz amewataka mafans wa lebo hiyo kukaa mkao wa kula
kutokana na mambo makubwa ambayo wameyaandaa ndani ya mwaka huu.
Nedy amefunguka huo mchongo wakati akipiga story na kipindi
cha Standard Mix cha Standard Radio jumanne hii,ambapo mkali alisema kuna ziara
imeandaliwa itakayomjumuisha yeye pamoja na Ommy Dimpoz, tour ambayo wamepanga kuzunguka mikoa mingi ndani
ya Bongo ambayo hawajawahi kufika na kutoa burudani kwa mashabiki wao huku wakiiwakilisha
lebo yao ya Pozi Kwa Pozi.
‘Kuna tour ambazo zimeandaliwa za mimi na Ommmy Dimpoz
ambazo tunatarajia kufika mikoa mingi ambayo bado hatujaipanga lakini ni mikoa
mingi ambayo tutafika’’alisema Nedy
Kwa upande mwingine Nedy Music amedai kuwa huwa anapata
shows kutoka kwa mapromota na mpaka sasa hivi kuna baadhi ya maeneo tiari yuko
na ratiba kwa ajili kuachia burudani.
“Siyo kwamba sipokei simu za show kwasababu kuna show now
zimeshaandaliwa ntafanya Dar, ntafanya Dodom,ntanfanya Mwanza nikishatoka pia
kuna show Zanzibar kwa hiyo hizo zote ni show ambazo tiar ziko katika mpangilio
wa ratiba yangu’’aliongeza mkali
Nedy Music kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake Rudi aliyomshirikisha mkali wa masauti kutoka
Malaika Band,Cristian Bella.
0 Comments