KRC Genk imeonyesha si timu ya mchezo baada ya kuitwanga
Athletic Bilbao ya Hispania kwa mabao 2-0 katika mechi ya Europa Cup.
Genk iliyokuwa nyumbani, ilipata bao katika kila kipindi huku
Mtanzania akiingia katika kipindi cha pili, ilikuwa dakika ya 56 na kuchangia
kupatikana kwa bao la pili.
Bao la kwanza lilifungwa na Jakub Brabec aliyeunganisha pasi
safi ya Leon Bailey katika dakika ya 40, wakaenda mapumziko wakiwa wanaongoza.
Samatta aliingia kuchukua nafasi ya Thomas Buffel katika dakika
ya 56 na kaanza kuonyesha cheche.
Dakika ya 83, Onyinye Ndindi alifunga bao la pili na kushindilia
msumari wa mwisho kwa Wahispania hao.
Bilbao ni kati ya timu zenye historia ya juu katika La Liga kwa
kuwa ni kongwe na haijawahi kuteremka daraja kutoka La Liga. Nyingine ambazo
hazijawahi kuteremka ni Real Madrid na Barcelona tu.
0 Comments