VIONGOZI WA CCM NGAZI ZA MATAWI KATA NA WILAYA SINGIDA WAHIMIZWA KUFANYA MAANDALIZI

Katibu wa CCM mkoa wa Singida Bi Merry Maziku akiwa ofisini 
Viongozi wa chama cha mapinduzi ngazi za matawi, kata na wilaya mkoani Singida wamehimizwa kufanya maandalizi ya uchaguzi wa chama na Jumuiya zake kwa mwaka 2017.
Ameyasema hayo katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Singida Bi.Merry Maziku wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Aidha Bi.Maziku amesema kuwa chama kihakikishe kinachagua na kupata viongozi bora wenye kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Pia amewataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na usawa pasipo kuangalia undugu,urafiki,ujamaa na ukabila kwa wote ni watanzania 

Hata hivyo amewahamasisha viongozi wa ngazi zote kuwahimiza wananchi juu ya swala zima la kilimo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments