Raisi Jonh Pombe Magufuli |
Baraza la Habari nchini Tanzania
limewasilisha kesi mahakamani kupinga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari
iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo Novemba mwaka jana.
Baraza hilo limewasilisha kesi hiyo katika Mahakama ya Afrika
Mashariki (EACJ) likishirikiana na mashirika mawili ya kutetea haki za
kibinadamu; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Mtandao wa Watetezi wa Haki
za Binadamu Tanzania.
Baraza hilo linaaka baadhi ya vifungu vya sheria, ambavyo
wanasema vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza vifutwe.
Wanasema vinakiuka matakwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo
zinataka nchi wanachama kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba wa
kuundwa kwa jumuiya hiyo.
"Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unahimiza umuhimu
wa kufuata kanuni za utawala bora, utawala wa kidemokrasia, utawala wa sheria,
uwajibikaji, uwazi, haki kwa wote, usawa wa kijinsia na kuheshimu haki za
binadamu," baraza hilo linasema kupitia taarifa iliyotiwa saini na katibu
mtendaji Kajudi Mukajanga.
"Tanzania inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha haki zote
zilizotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa."
0 Comments