Raisi Dkt J.p.Magufuli na mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 24
Desemba, 2016 amewasili mkoani Singida na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa huo Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi mbalimbali wa
mkoa wa Singida.
Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, kesho tarehe 25 Desemba 2016 wanatarajia
kuungana na waumini wengine wa dini ya Kikristo nchini katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi mkoani
Singida.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaomba waumini wa
dini ya kikristo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kuungana na Rais Magufuli katika ibada ya
Krismasi kwani imekuwa ni heshima kwao kutokana na uwepo wa Rais Mkoani hapa kwa ajili ya sikukuu ya
Krimass.
Dkt.
Nchimbi amewataka wananchi wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kuendelea
kumuombea Rais Magufuli na familia yake ili aendelee kuwatumikia watanzania katika
kuwaletea maendeleo.
Amesema
ni bahati kubwa kwa mkoa wa Singida kwa mara nyingine tena kumpokea Kiongozi
huyo Mkuu wa nchi kwa kuwa katika kipindi kifupi mkoa huo pia ulimpokea Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa
alipohudhuria sherehe za Maulidi.
Jaffar
Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Singida
24
Desemba, 2016
0 Comments