Wapatanishi katika Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo, wameandaa mwafaka wa
kuhakikisha kuwa madaraka yanapokezwa kwa njia ya amani.
Mashauriano
yaliyoandaliwa na Kanisa Katoliki, yanafuatia kukataa kwa Rais Joseph Kabila,
kuondoka madarakani baada ya utawala wake wa mihula miwili kukamilika.
Chini ya mapatano hayo Rais Kabila ataendelea kuwa Rais hadi
wakati wa uchaguzi ifikapo mwisho wa mwaka ujao.
Waziri Mkuu mpya
atachaguliwa kutoka kwa upande wa upinzani na mpango huo utasimamiwa na mkongwe
wa upinzani, Etienne Tshisekedi.
Mwandishi wa habari
wa BBC, alisema kuwa ingawa kuna ripoti kuwa pande kinzani zimekubaliana kwa
maswala fulani, haiwezekani sahihi za mkataba huo kutiwa sahihi kabla Krismasi.
Kukataa kwa Bwana Kabila kuondoka madarakani na kuahirishwa kwa
uchaguzi kumesababisha maandamano makali katika barabara kuu za miji nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
0 Comments