KIUNGO wa zamani wa Azam, Jean Babtiste Mugiraneza 'Migi' amesaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea Gor Mahia ya Kenya akichukuwa nafasi ya
Khalid Aucho aliyeenda kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.
Migi ambaye walifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Azam alisafiri
jana kwenda kusaini mkataba huo jijini Nairobi na kurudi Dar es Salaam
kuendelea kufuatilia haki zake.
Migi anawadai Azam mshahara wa miezi nane ambapo anapaswa kulipwa dola
24000 kwani mshahara wake ni dola 3000 kwa mwezi.
Meneja wa mchezaji huyo Claver Kazungu Amesema kuwa baada ya kumalizana
na Azam mteja wake atarejea kwao Rwanda ndipo aende kujiunga na Gor Mahia ambao
kwa sasa wapo kwenye mapumziko baada ya ligi kumalizika.
Migi ameigomea ofa aliyopata kutoka timu ya Than Quang Ninh inayoshiriki
ligi ya Vietnam ambayo alitafutiwa na Mtendaji Mkuu, Saady Kawemba.
Imeelezwa kuwa Gor Mahia imesajili pia
beki wa kushoto Abubakar Sibomana na mshambuliaji Jack Tuyisenge wote raia wa
Rwanda ambao wanachezea timu ya APR.
0 Comments