Jaffar Iddi Maganga |
WINGA wa timu ya Azam FC Farid Mussa ataondoka nchini kesho usiku
kuelekea Hispania baada ya kutumiwa tiketi ya ndege na klabu ya Tenerife
inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.
Faridi ataondoka kesho saa 5 usiku kwa ndege ya KLM ampapo atapitia
Amsterdam, Barcelona hadi kufika Tenerife ambapo atajiunga na miamba hiyo kwa
mkopo baada ya danadana za muda mrefu kuhusu safari yake.
Awali Tenerife
walitaka kumsajili winga huyo kwa mkataba wa moja kwa moja baada ya kufaulu
majaribio lakini dau ambalo walitaka kutoa lilikataliwa na Azam kwakua lilikuwa
dogo kabla ya kukubaliana kumchukua kwa mkopo.
Ofisa Habari wa timu hiyo Jaffar Iddi Maganga amewaonyesha Waandishi wa
Habari tiketi hiyo huku akisema kuondoka kwa winga huyo kutafungua milango kwa
wachezaji wengine wa Tanzania kwavile atautangaza vyema mpira wa nchi hii.
"Kesho saa 5 usiku mchezaji wetu Farid ataondoka nchini kuelekea
Hispania kwa ndege ya KLM kujiunga na timu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja
la pili na tayari ametumiwa tiketi kwa ajili ya safari hiyo na sisi Azam
tunamtakia kila la kheri katika maisha mapya ya soka" alisema Maganga.
Azam watalipa
stahiki zote za mchezaji huyo ikiwemo mshahara kwa mujibu wa mkataba
walioingia na klabu hiyo ya Hispania.
0 Comments