Singida
Katika
kuelekea maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu, michezo mbalimbali inaendelea
kufanyika mkoani Singida. Miongoni mwa michezo hiyo ni riadha maalum kwa wazee
wenye umri wa kuanzia miaka 50.
Mbio hizo,
zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mwenge, zimevutia mashabiki
wengi baada ya wazee, wa kiume na wa kike, kutimua vumbi katika mbio za mita
100. Bingwa mtetezi kwa upande wa wanawake ameendeleza ubabe wake kwa kutetea
taji alilolitwaa Mei Mosi mwaka 2024.
Baada ya
kumaliza mashindano hayo, wazee hao walizungumza juu ya umuhimu wa kufanya
mazoezi katika kuimarisha afya ya mwili wa binadamu.
0 Comments