VETA YASHEHEREKEA MIAKA 30 KWA KUJENGA VYUO VIPYA NA KUBORESHA AJIRA

 

Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi nchini Anthony Kasore anikongea na waandishi wa Habari juu ya Naadhimisho ya Miaka 30 ya Veta mjini Singida.








picha za matukio mbalimbali ya uzinduzi wa kuelekea maadhimisho ya Miaka 30 ya Veta Mkoani Singida


Singida

Na Mwandishi Wetu

serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania imepanga kujenga vyuo vipya 65 vya mamlaka ya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (veta) katika mikoa mbalimbali nchini. hatua hii inalenga kuongeza fursa za elimu ya ufundi kwa vijana na kuinua viwango vya ujuzi ili kuboresha ajira na kujiajiri kwa watanzania.

akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya veta, yaliyofanyika katika ukumbi wa veta mkoani singida, mkurugenzi mkuu wa veta, cpa anthony mzee kasore, amesema kuwa ujenzi wa vyuo hivyo utachochea maendeleo kwa kuwapa mafunzo bora wahitimu wengi zaidi.

"kwa sasa, veta ina vyuo 80 ambavyo vinadahili jumla ya wanafunzi 83,974 kwa mwaka, tofauti na ilipoanzishwa mwaka 1995 ambapo kulikuwa na vyuo 14 pekee vilivyokuwa vinadahili wanafunzi 1,940. ujenzi wa vyuo 65 vipya utaongeza udahili wa zaidi ya wanafunzi 80,000, hatua inayolenga kupunguza ukosefu wa ajira nchini," amesema cpa kasore.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments