Picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika maadhimisho ya kanda ya Kati ya Veta
Singida
Na Mwandishi Wetu
Wito umetolewa kwa Vijana wanaomaliza masomo yao katika vyuo vikuu na vya kati wamehimizwa kujiunga na vyuo vya ufundi stadi ili kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri na kuimarisha maisha yao kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, alitoa wito huo alipofunga maadhimisho ya miaka 30 ya VETA na miaka 50 ya utoaji wa elimu ya ufundi stadi Kanda ya Kati. Amesema mkoa umejipanga kuweka mikakati madhubuti ili kuwawezesha vijana kupata ujuzi huo kwa urahisi.
Aidha, Dendego alipongeza vyuo vya VETA kwa mchango wao mkubwa katika kuwaandaa vijana kupitia mafunzo ya vitendo. Akiwa katika ziara, alitembelea ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida, unaotekelezwa na mafundi waliopitia VETA, na kuwasisitiza vijana kujiunga na vyuo hivyo ili kuongeza maarifa yao ya ufundi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa VETA
Kanda ya Kati, Ramadhani Makata, alisema serikali imeendelea kuboresha
mazingira ya elimu ya ufundi kwa kuhakikisha mafunzo hayo yanapatikana kwa
gharama nafuu. Alibainisha kuwa zaidi ya shilingi bilioni 27 zinatumika katika
ujenzi wa vyuo 18 vya VETA katika mikoa ya Dodoma, Singida, na Manyara, ambapo
vyuo tisa tayari vimekamilika.
0 Comments