Singida
26.2.2025
Maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yamezinduliwa jana, Februari 25, 2025, katika viwanja vya Bombadia, Mjini Singida, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe. Maadhimisho haya yatafikia kilele chake Februari 27, 2025, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Katika hotuba yake, Mhe. Gondwe amewahimiza wazazi kutumia fursa za Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) ili kuwapa vijana wao elimu itakayowawezesha kujiajiri. Ameitaka VETA Kanda ya Kati kushirikiana na viwanda vya Singida ili kuongeza ujuzi wa vitendo kwa wanachuo.
Mbunge wa Jimbo la Singida, Mhe. Musa Sima, amesisitiza umuhimu wa kutambua vijana walioko mtaani wenye ujuzi wa ufundi na kuwapatia vyeti rasmi ili kuwawezesha kupata fursa zaidi za ajira. Pia, Serikali imewataka wahitimu wa vyuo vikuu kujiunga na VETA ili kujifunza ujuzi wa vitendo badala ya kutegemea ajira za ofisini pekee.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati, Ramadhani Makata, amewahimiza vijana kujiunga na vyuo vya ufundi stadi kama njia ya kujikwamua kiuchumi.
Katika
maonesho haya, jumla ya vyuo tisa vya VETA kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, na
Manyara vinashiriki, yakilenga kuonyesha mchango wa elimu ya ufundi stadi kwa
maendeleo ya taifa.
0 Comments