FAINALI YA KWANZA YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA




FAINALI ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika inafanyika leo Uwanja wa Lucas Moripe mjini Johannesburg, Afrika Kusini kati ya wenyeji, Mamelodi Sundowns na Zamalek ya Misri kuanzia 10:00 jioni.

Timu hizo zitarudiana Ijumaa ya Oktoba 21, mwaka huu Zamalek wakiwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns katika mechi ya Kombe uwanjani mjini Cairo, Misri.

Zamalek iliingia Fainali baada ya kuitoa Wydad Casablanca kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 4-0 nyumbani Cairo na kufungwa 5-2 ugenini Casablanca. 

Mamelodi iliitoa Zesco United kwa jumla ya mabao 3-2 ikishinda 2-0 nyumbani baada ya kufungwa 2-1 Zambia.
Mabingwa wa Afrika msimu uliopita, TP Mazembe ya DRC mwaka huu hawakufuzu hatua ya makundi baada ya kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho.

Hata hivyo, katika michuano hiyo midogo ya klabu barani, Mazembe imefanikiwa kufika fainali ambako itamenyana na MO Bejaia ya Algeria Oktoba 29 katika kabla ya kurudiana Novemba 6, mwaka huu.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments