CHAMA CHA WACHIMBAJI WADOGO MKOA WA SINGIDA (SIREMA) CHAPATA UONGOZI MPYA

Bw Robart Marando akiongea baada ya kutetea nafasi yake ya uwenyekiti wa wachimbaji mkoa wa Singida (SIREMA)

Katibu mkuu mteule Bw Farijara Kiunsi akitoa shukrani zake kwa wanachama kwa kuendelea kumwamini katika nafasi yake ya katibu mkuu wa (SIREMA).
Bi Matha Alex kushoto na kamishina Masolwa katikati kulia ni mwenyekiti Bw Robert Malando 
Katubu mkuu wa (SIREMA) Bw Farijara Kiunsi  taarifa ya chama kabla ya kuanza uchaguzi huo
Kamishina wa madini kanda ya kati Bw Masolwa aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi na mgeni rasimi akiongea na wanachama wa chama hicho cha wachimbaji mkoa wa Singida (SIREMA) kabla ya kuanza zoezi la uchaguzi.

Wasimamizi wa uchaguzi huo wa ngazi ya mkoa wa Singida wakiongozwa na kamishina wa madini  mkoa wa Singida  Bw Masolwa katikati.

CHAMA cha wachimbaji wadogo wa madini (SIREMA) Mkoa wa Singida kimefanya uchaguzi na kupata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ofisi za idara ya madini kanda ya kati,BW ROBERT MARANDO alifafaanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti baaada ya kupata kura zote 16.

Makamu Mwenyekit Sheikh Yahaya Ibrahimu alipata kura 16 za ndiyo wakati katibu Mkuu FARIJALA KIUNSI alipata kura za ndiyo 14 na kura za hapana 2,,Mhasibu mkuu YUSUFU KIBILA alipata kura zote 16 za ndiyo,Mhasibu msaidizi BERTHA MKUMBO alipita bila kupingwa.

Katika uchaguzi huo pia walichaguliwa wajumbe wa FEMATA TAIFA kuwa ni JOHN BINA,JOHN METTA(Wafanyabiashara wa madini)MARTHA ALEX NDUNGURU(wanawake FEMATA),INNOCENT HUGO MAKOME(Wachimbaji wasio na leseni (FEMATA)

WAJUMBE wa kamati ya Utendaji ni Magdalena Lucas(mama boke),GRETEA NGOI,PILI(MAMA PILI)

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments