SINGIDA
Mashindano
ya kuelekea kilele cha Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) yameendelea kwa
shamrashamra katika viwanja vya Bombadia, mjini Singida, ambapo timu mbalimbali
kutoka wizara za serikali zimekutana kwenye mchezo wa kuvuta kamba.
Mashindano
hayo ambayo yamejumuisha wizara na taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara ya
Utalii, Viwanda na Biashara, Ujenzi, Tanesco, Mambo ya Nje, Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Singida, Ikulu na Mambo ya Ndani, yamekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi
wa Singida na washiriki wenyewe.
Kwa siku ya
leo, pambano lilihusisha timu za wanaume ambapo mvutano mkali ulijitokeza kati
ya timu za Utalii, Ikulu na Mambo ya Ndani. Timu hizi zilionyesha ushindani wa
hali ya juu, huku wachezaji wakionesha nidhamu, uimara na mbinu mbalimbali za
kuibuka kidedea. Timu ya Mambo ya Ndani ilionyesha ubabe kwa kuibwaga timu ya
Ikulu katika moja ya michezo iliyokuwa na ushindani mkali na wa kusisimua.
Mchezo wa
kuvuta kamba unatarajiwa kuendelea katika siku zijazo kwa kushirikisha pia timu
za wanawake, ambapo kila timu inapambana si tu kwa lengo la ushindi, bali pia
kuonesha mshikamano na kuhamasisha afya na ushirikiano kazini.
Mashindano
haya yamepangwa kuanza kila siku saa 12:30 asubuhi, yakihamasisha mwamko wa
michezo na ushiriki wa taasisi mbalimbali katika kuelekea sherehe za Mei Mosi
kitaifa.










0 Comments