Sibgida
(picha na matukio mbalimbali)
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amefungua rasmi
Mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari wa Kanda ya Kati katika Ukumbi wa TIA –
Singida.
Katika hotuba yake, Mhe. Dendego amesisitiza umuhimu wa
maadili, uzalendo na uwajibikaji mashuleni, akihimiza walimu kuwa mstari wa
mbele kupambana na changamoto kama utoroshaji, mimba za utotoni na kushuka kwa
nidhamu.
“Tukilea wanafunzi
kimaadili, tunajenga viongozi wa baadaye.” – RC Dendego
Aidha, amewapongeza wakuu wa shule kwa kusimamia kwa
mafanikio miradi ya elimu chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, na kuwakumbusha
kuhusu ushiriki wa walimu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Mei Mosi
yatakayofanyika hapa Singida.
Mkutano huu wa siku
mbili unaleta pamoja wakuu wa shule kutoka Singida na Dodoma kujadili uongozi,
TEHAMA, mazingira ya kujifunzia, na maboresho ya kitaaluma kupitia TAHOSA.
0 Comments