Mkuu wa mkoa wa Singida Akikabidhi msaada mablimbali kwaajiri ya wagonjwa waliyolazwa katika hosptali ya Rufaa Mandewa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akinda mti ikiwa ishara ya kuunga mkoano jitihada za serikali katika kutunza nazingila
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata akipanda mti katika maadhimisho ya miaka ya 63 ya uhuru.
Na Mwandishi Wetu
Mkoa wa Singida umeadhimisha miaka 63 ya Uhuru kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwa ni pamoja na kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mandewa na kutoa misaada kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya kina mama. Katika juhudi za kuimarisha uhifadhi wa mazingira, miti zaidi ya 500 ilipandwa katika eneo la hospitali hiyo, hatua inayolenga kuboresha mazingira na afya ya jamii.
Maadhimisho hayo yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Mheshimiwa Halima Dendego, ambaye kwa furaha pia alisherehekea siku yake ya
kuzaliwa. Mheshimiwa Dendego aliandamana na viongozi wa chama na serikali,
wakiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Martha Mlata, wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi ya Mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa
halmashauri, pamoja na wanahabari na wananchi kwa ujumla.
Kwa niaba ya mgeni rasmi wa maadhimisho hayo kimkoa, Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa alihimiza
wananchi kudumisha amani, mshikamano, na usafi wa mazingira. Pia aliwataka
wakulima kuchukua fursa ya mvua zinazonyesha kwa kupanda miti na kuimarisha
kilimo, akibainisha kuwa serikali imeendelea kuboresha upatikanaji wa pembejeo
kupitia ruzuku ya mbegu na mbolea ili kuongeza uzalishaji.
Naye Chief Senge wa Singida pamoja na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mheshimiwa Elia Digha,
walipozungumzia maendeleo yaliyopatikana katika miaka 63 ya Uhuru, walisema
kuwa mafanikio haya yanadhihirisha umuhimu wa amani na utulivu wa nchi chini ya
uongozi bora wa taifa hili.
Maadhimisho haya yameonyesha mshikamano wa viongozi na
wananchi wa Singida katika kusherehekea uhuru kwa vitendo vinavyolenga
kuimarisha maisha ya jamii na ustawi wa mkoa huo.
0 Comments