Baada ya maeongezi na makabidhiano ya mihuri yakafanyika maongezi ya kubadilishana mawazo kabla ya kikao cha WODC.kufanyika.
Singida,
Desemba 2, 2024 –
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Singida na Diwani wa Kata ya Majengo, Mhe. Yagi Maurid
Kiaratu, amekabidhi mihuri kwa wenyeviti wa mitaa ya kata hiyo katika hafla
maalum iliyofanyika leo. Akizungumza na viongozi hao, Mhe. Kiaratu alitoa wito
kwa wenyeviti hao kushirikiana kikamilifu kuhakikisha maendeleo ya Kata ya
Majengo, ambayo ipo katikati ya mji wa Singida, yanazingatia ustawi wa wakazi
na mwonekano wa kisasa wa eneo hilo.
Mhe. Kiaratu alihimiza umuhimu wa kuja
na mtazamo wa ujenzi wa majengo mapya ili kuboresha miundombinu na kuendana na
kasi ya ukuaji wa mji wa Singida. Aidha, alisisitiza jukumu la wenyeviti wa
mitaa katika kusimamia usafi wa mazingira, kudumisha usalama, kushughulikia
migogoro ya kijamii kwa njia za amani, na kuepusha migongano baina ya watendaji
na wenyeviti.
“Tunataka kuona kazi inafanyika kwa
umoja na mshikamano. Migongano ya mara kwa mara haiwezi kutuletea maendeleo
tunayoyahitaji. Mtu wa Majengo anatakiwa kufurahia maisha bora, usalama, na
mazingira safi,” alisema Mhe. Kiaratu.
Aidha, alitoa changamoto kwa wenyeviti
kuonyesha uongozi wa mfano kwa kushirikiana na wananchi katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo. Aliongeza kuwa, manispaa iko tayari kutoa msaada wa
kiufundi na ushauri pale inapohitajika, lakini wenyeviti wanapaswa kuchukua
hatua za awali kuibua na kutekeleza mawazo chanya yanayochochea maendeleo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watendaji
wa serikali, viongozi wa kata, na baadhi ya wananchi waliotumia fursa hiyo
kupongeza juhudi za Mhe. Kiaratu katika kuleta mabadiliko katika kata ya
Majengo na manispaa kwa ujumla.
0 Comments