Na Mwandishi wetu
-Singida
WAKAZI wawili wa mkoa wa Mwanza wanaotuhumiwa kuua walinzi
wawili wa usiku katika manispaa ya
Singida na kuwapora/kunyang’anya simu nne za vingajani,wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani agosti 19 mwaka huu.
Watuhumiwa hao ni Chacha Marwa Sandu ambaye pia anatambulika kwa
majina ya Jose Samwel S.Mgosi Mkurya.na mtuhumiwa mwingine ni Michael Steven
Mkono au Kipara.
Chacha mwenye umri wa miaka 24,ni mchimba madini,wakati Michael
mwenye umri wa miaka 45,ni mfanyabiashara Burugu.
Washitakiwa hao wanashitakiwa kwa kosa la mauaji kulingana na
kifungu namba 196 na 107, ya kanuni ya adhabu (cap 16,2022).
Wanadaiwa kuwa aprili 19 mwaka huu,wakiwa mtaa wa Salimini
kata ya Misuna kata ya Mungu Maji manispaa ya Singida.Majira ya usiku,walimuua
Leonce Ilanda Njiku.Wakati alipokuwa kwenye lindo lake.
Imeelezwa kwamba baada ya kuhakikisha wamemuua mlinzi
huyo,walimpora simu zake mbili za kigajani.
Usiku ule ule wa aprili 19 mwaka huu,washitakiwa hao walimuua
Isamail Ramadhani mkazi wa Ng’ongoajibu mtaa wa Majengo kata ya Mungu Maji.
Walitekeleza unyama huo usiku Ramadhani akiwa kwenye ulinzi
wa ghala,na kumpora simu mbili pia za kiganjani.
Wajibu wa mahakama ya mkoa,ni kutaja tu tarehe ya kufikishwa
mahakamani kwa watuhumiwa. .Mahakama kuu ndiyo yenye mamlaka ya
kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Singida SACP Amon
Kakwele,amesema kuwa baada ya watuhumiwa kutokomea kusikojulikana,jeshi la
polisi Singida likishirikiana na kitengo cha uchunguzi wa matukio kisayansi na
makosa ya mtandao,walibaini watuhumiwa wamekimbilia mikoa ya Mwanza,Simiyu na
Shinyanga.
“Timu ya makachero kutoka Singida ilitumwa na ambapo watuhumiwa
hao walikamatwa mei 26 mwaka huu huko wilayani Kahama mkani Shinyanga.Upelelezi
kwa sasa umekamilika na watuhumiwa tayari wameishafikishwa mahakamani”,alisema
SACP Kakwale.
Aidha amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na jeshi
la polisi mkoa wa Singida,kutoa taarifa kupitia ofisi za kituo
kidogo cha polisi stand ya zamani,na kata.
Kamanda huyo ametumia fursa hiyo kuwashukru wananchi wema kwa
msaada wao uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kikao cha wadau wa usalama na jeshi la polisi kilichofanyika
muda mfupi baada ya matukio hayo.Ndicho kilichofanikisha kukamatwa kwa
watuhumiwa na sheria inachukua mkondo wake.Tunawaomba waendelee kushirikiana
polisi bega kwa bega .
0 Comments