Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Singida na Diwani wa kata ya Mudida Mhe Omary Mande akifungua kikao cha Baraza la madiwa ikiwa ni siku ya kwanza ya kikao hicho kilicho dadili juu ya mapato ya kata katika Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Singida Ester Chaula akisimamam kutolea ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizotolewa na madiwani katika siku ya kwanza ya kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika katika ukumbi wa ofisi ya Halmashauri Ilongero.
Mhe Issa Mwiru diwani wa kata ya Ilongero akiwasilisha hoja katika baraza la Madiwani wilaya ya Singida Juu ya ukusanyaji wa Mapato.
Mhe Jumanne Jambi diwani wa kata ya Makuro akitoa hoja juu ya mapato ya kata ya hiyo na Halmashauri.
Diwani wa kata ya Mtinko Bilali Yusuph alipata fursa ya kuchangia hoja iliyoletwa juu ya baadhi ya kata kuto fanya vyema katika makusanyo ya mapato ya Halmashauri.
SINGIDA
Na Cales katemana
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula, ameeleza kuwa mfumo wa mauzo ya mazao kupitia stakabadhi ghalani umeleta mafanikio makubwa kwa halmashauri, ambapo zaidi ya shilingi milioni 200 zimekusanywa kwa mara ya kwanza. Mfumo huo umetumika katika kata za Mwasauya, Msange, Mudida, na Mtingo.
Chaula amewataka watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanasimamia kwa ufanisi ukusanyaji wa mapato licha ya changamoto zilizopo, zikiwemo ukosefu wa miundombinu bora na upungufu wa watendaji.
Aidha, akijibu hoja za madiwani kuhusu uzembe wa baadhi ya watendaji, ikiwemo kushindwa kuwasilisha fedha za mapato benki kwa wakati, Chaula amesema serikali ina mpango wa kuajiri watendaji wa vijiji katika halmashauri hiyo ili kumaliza changamoto ya kaimu watendaji.
"Ni muhimu kila mtendaji ahakikishe mapato yanakusanywa kwa ufanisi na yanapelekwa benki kwa wakati ili kuimarisha maendeleo ya wilaya yetu," alisisitiza.
Halmashauri
ya Wilaya ya Singida inaendelea kusisitiza uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu
kwa manufaa ya wananchi wote.
0 Comments