WATHIBITI UBORA WA SHULE 378 WAPATIWA MAFUNZO YA ELIMU JUMUISHI SINGIDA




Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa shule (MUS) Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia Ephraim Simbeye akifungua mafunzo hayo ya Siku tatu yanayofanyika Mkoani Singida katika ukumbi wa chuo cha ufundi VETA.



Meza kuu ikiwa na wakuu wa idara na wakurugezi mbalimbali kutoka Tamisemi na wizarani wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi.



Maofisa kutoka makao makuu na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika ukumbi wa chuo cha ufundi Veta Singida.


Singida, 13 Novemba 2024 – 

Wathibiti ubora wa shule 378 kutoka Halmashauri 92 nchini wamepata mafunzo maalum ya siku tatu kuhusu utekelezaji wa kiunzi cha elimu jumuishi kwa shule za awali na msingi. Mafunzo haya yanalenga kuboresha sekta ya elimu ili kukidhi mahitaji ya maendeleo endelevu na kuimarisha ushirikishwaji wa wanafunzi wote.

Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia, Ephraim Simbeye, alifungua rasmi mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Singida. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Simbeye alisisitiza umuhimu wa programu hiyo mpya kama njia ya kukabiliana na changamoto ya mdondoko wa wanafunzi.

“Lengo ni kuhakikisha kuwa elimu ya awali na msingi inakuwa jumuishi, na tunawahimiza wathibiti kutumia nafasi zao kushirikiana kwa karibu na viongozi wapya katika utekelezaji wa mikakati hii muhimu,” alisema Simbeye.

Baadhi ya washiriki waliopata nafasi ya kuzungumza walipongeza juhudi za serikali kwa kutoa mafunzo hayo, wakibainisha kuwa mafunzo haya yatasaidia kuboresha utendaji wao na kuhakikisha utekelezaji mzuri wa elimu jumuishi katika shule walizopo.

Mafunzo haya yanatarajiwa kutoa mwanga mpya katika kuhakikisha kuwa shule za awali na msingi zinakuwa sehemu salama na zenye usawa kwa wanafunzi wote, bila kujali mahitaji yao maalum.















Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments